Date: 
11-11-2025
Reading: 
Mhubiri 8:11-13

Jumanne asubuhi tarehe 11.11.2025

Mhubiri 8:11-13

11 Kwa sababu hukumu juu ya tendo baya haitekelezwi upesi, mioyo ya wanadamu huthibitishwa ndani yao ili kutenda mabaya.

12 Ajapokuwa mwenye dhambi amefanya maovu mara mia, akazidisha siku zake; lakini hata hivyo najua hakika ya kwamba itakuwa heri kwao wamchao Mungu, wenye kicho mbele zake;

13 walakini haitakuwa heri kwa mwovu, wala hatazidisha siku zake, zilizo kama kivuli; kwa sababu hana kicho mbele za Mungu.

Tuvumilie hata mwisho katika Bwana;

Tunamsoma Suleimani akiwa na maudhui kwamba njia za Mungu hazichunguziki. Suleimani anaeleza kwamba mwanadamu akitenda jambo baya atahukumiwa kwa sheria za mahali husika. Lakini Mungu ni wa pekee, kwamba mtu akikosa akaomba msamaha, anasamehewa. Mungu haoni heri kwa mwovu asiyetubu, maana leongo lake ni wote wafike kwake.

Leo asubuhi Suleimani anatukumbusha kwamba tuishi maisha ya toba, maana yeye hutaka watu wake watubu. Petro anaandika katika waraka kuhusu Bwana atakavyo watu watubu;

2 Petro 3:9

Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba.

Wito wangu kwako asubuhi hii ni kuhakikisha umesamehewa dhambi zako kabla hujalala. Huko ndiko kuvumilia kwenyewe kuelekea uzima wa milele. Amina

Jumanne njema

 

Heri Buberwa Nteboya 

0784 968650 

bernardina.nyamichwo@gmail.com