Date: 
18-08-2025
Reading: 
Mithali 9:9-12

Jumatatu asubuhi tarehe 18.08.2025

Mithali 9:9-12

9 Mwelimishe mwenye hekima, naye atazidi kuwa na hekima; Mfundishe mwenye haki, naye atazidi kuwa na elimu;

10 Kumcha Bwana ni mwanzo wa hekima; Na kumjua Mtakatifu ni ufahamu.

11 Maana, kwa msaada wangu siku zako zitazidishwa; Na miaka ya maisha yako itaongezwa.

12 Kama una hekima, una hekima kwa nafsi yako; Na kama una dharau, utaichukua peke yako.

Tuenende kwa hekima ya Mungu;

Suleimani katika sura ya 9 anaongelea hekima ya Mungu ifaayo kwa wanadamu. Suleimani anawaita wasio na hekima ya Mungu "wajinga" maana hawawezi kuamua na kutenda kama Mungu atakavyo. Katika somo la asubuhi hii, Suleimani anasema kuwa mwenye hekima akielimishwa huzidi kuwa na hekima maana huelewa zaidi, mwenye haki vivyo hivyo. Kumbe hekima ya Mungu ni muhimu kwetu, maana hutufanya kumfuata Bwana atakavyo.

Mkazo wa Suleimani katika somo la asubuhi ya leo ni kwamba kumcha Bwana ni mwanzo wa hekima. Kwa njia hiyo anawaita waaminio kukaa katika imani kwa njia ya neno la Mungu, maana neno ndilo hutuwezesha kuwa na hekima itokayo kwa Mungu. Hekima ya kweli yatoka kwa Yesu Kristo. Mwamini sasa uokolewe. Amina

Uwe na wiki njema kwa hekima ya Mungu. 

 

Heri Buberwa Nteboya 

0784 968650 

bernardina.nyamichwo@gmail.com