Date:
14-12-2024
Reading:
Isaya 51:1-3
Hii ni Advent;
Jumamosi asubuhi tarehe 14.12.2024
Isaya 51:1-3
[1]Nisikilizeni, ninyi mnaoifuatia haki; ninyi mnaomtafuta BWANA; uangalieni mwamba ule ambao mlitolewa kwa kuchongwa, na tundu la shimo ambalo mlitolewa kwa kuchimbuliwa.
[2]Mwangalieni Ibrahimu, baba yenu, na Sara, aliyewazaa; kwa maana alipokuwa mmoja tu nalimwita, nikambariki, nikamfanya kuwa wengi.
[3]Maana BWANA ameufariji Sayuni; amepafariji mahali pake palipokuwa ukiwa; amefanya jangwa lake kuwa kama bustani ya Edeni, na nyika yake kama bustani ya BWANA; furaha na kicheko zitaonekana ndani yake, kushukuru, na sauti ya kuimba.
Ukombozi wetu umekaribia;
Nabii Isaya anatoa unabii juu ya baraka zilizowekwa kwa ajili ya Taifa la Mungu. Anatoa mfano wa Ibrahimu aliyeitwa, akaitika, akabarikiwa. Anatoa ujumbe wa furaha na kicheko kwa watakaompokea Bwana.
Yesu anatuita kumpokea, ili atubariki. Tunapongojea kurudi kwake, tumuige Ibrahimu, yaani tuikitike wito wake kwa kumfuata, ili ajapo tuingie katika ufalme wake. Amina
Uwe na Jumamosi njema
Heri Buberwa
Mlutheri