MATANGAZO YA USHARIKA  

TAREHE 20 OKTOBA, 2024

SIKU YA BWANA YA 21 BAADA YA UTATU 

NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI

TUISHINDANIE IMANI KATIKA KRISTO YESU 

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Hakuna .mgeni aliyetufikia kwa cheti. 

3. Matoleo ya Tarehe 13/10/2024

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 mchana. Alhamisi saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV.

5. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana hapo nje na kwenye duka letu la vitabu kwa bei yaTsh. 40,000/=. 

6. Kamati ya Afya na Ustawi wa jamii inapenda kuwatangazia kuwa mafundisho ya afya kwa wanafunzi wa Kipaimara kwa Mwaka wa Kwanza na wa pili yatafanyika tarehe 16/11/2024 kuanzia saa 2.00 asubuhi mpaka saa 9.00 alasiri hapa Usharikani. Wale waliopata Kipaimara wenye umri wa miaka 15 pia wanakaribishwa kwenye mafundisho haya. Wazazi na Walezi mnaombwa kuandikisha watoto watakaohudhuria kwa Parish Worker ili kufanya maandalizi haya.

7. Jumapili ijayo tarehe 27/10/2024 tutashiriki chakula cha Bwana. Washarika tujiandae.

8. Shukrani: Jumapili ijayo tarehe 27/10/2024 katika

Ibada ya Kwanza saa 1:00 asubuhi, 

  • Familia ya Mzee Happiness Nkya watamshukuru Mungu kwa mambo makuu aliyowatendea ikiwamo ulinzi na faraja katika kipindi cha miaka 20 tokea mpendwa wao Mama Festasia Nkya alipotwaliwa kutoka katika maisha haya. Pamoja na Rosemary Nkya, Nadia kukumbuka siku zao za kuzaliwa. 

Neno: Zab 125:1-2 , Wimbo TMW 49. Nakutegemea Yesu.

9. Umoja wa Vijana Watamshukuru Mungu kwa kuwapa kibali na kuwawezesha kufanya ibada ya mkesha “The Night of Praise” Season 2 ambao ulifanyika tarehe 04/10/2024 pia kutoa shukrani zao kwa washrika waliowawezesha katika maandalizi ya ibada na kushiriki katika ibada.

Neno: Zab 33:2-4 , Wimbo: Bwana nimerudi tena(Praise Team)

10. NDOA: NDOA ZA WASHARIKA 

Ndoa za Washarika

KWA MARA YA PILI TUNATANGAZA NDOA YA TAREHE 02/11/2024

SAA 4.00 ASUBUHI

Bw. Noel Ponesya Kaminyoge na Grace Paul Marcus

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu. 

11. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

  • Upanga: Kwa Mama Ndossi
  • Mjini kati: Watafanyika hapa usharikani jumamosi saa 1.00 asubuhi 
  • Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Mama Mamkwe.
  • Kinondoni: Kwa Bwana na Bibi Danford Mariki
  • Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bwana na Bibi Frank Korassa
  • Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach: Kwa Mama Vicky Makani
  • Ilala, Chang’ombe, Buguruni: Kwa Bwana na Bibi Kelvin Matandiko
  • Oysterbay, Masaki: Kwa ………………..

12. Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la Pili.  

Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.