Date: 
27-12-2021
Reading: 
Mathayo 2:19-23

Jumatatu asubuhi tarehe 27.12.2021

Mathayo 2:19-23

19 Hata alipofariki Herode, tazama, malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto huko Misri,
 
20 akasema, Ondoka, umchukue mtoto na mamaye, ushike njia kwenda nchi ya Israeli; kwa maana wamekufa walioitafuta roho ya mtoto.
 
21 Akaondoka akamchukua mtoto na mamaye, akafika nchi ya Israeli.
 
22 Lakini aliposikia ya kwamba Arkelao anamiliki huko Uyahudi mahali pa Herode babaye, aliogopa kwenda huko; naye akiisha kuonywa katika ndoto, akasafiri pande za Galilaya,
 
23 akaenda, akakaa katika mji ulioitwa Nazareti; ili litimie neno lililonenwa na manabii, Ataitwa Mnazorayo.

Stefano shahidi mwaminifu wa Yesu;

Baada ya Herode kufariki Yusufu anaelekezwa kurudi toka Misri alipoenda kumficha Yesu ili asiuawe na Herode. Kuanzia kumchukua Mariamu akiwa mjamzito, kwenda Misri na kurudi, pote aliisikiliza sauti ya Mungu.

Tunaweza kuwa mashahidi wa imani kwa kuisikia na kuitii sauti ya Mungu, kwa mfano wa Yusufu. Utii wa Yusufu ulisababisha Yesu asiuawe. Kumbe nasi tukiwa watii tunailinda imani yetu katika Kristo, kama Stefano alivyosimama hadi mwisho akimtetea Kristo. Mtetee Kristo kwa kumsikiliza na kumtii.

Uwe na wiki njema