IJUMAA TAREHE 24 SEPTEMBA 2021, ASUBUHI.
Isaya 57:16-19
16 Kwa kuwa sitashindana na watu siku zote, wala sitakuwa na hasira siku zote; maana roho ingezimia mbele zangu, na hizo nafsi nilizozifanya.
17 Kwa sababu ya uovu wa kutamani kwake naliona hasira, nikampiga; nalificha uso wangu, nikaona ghadhabu; naye akaendelea kwa ukaidi, kuifuata njia ya moyo wake mwenyewe.
18 Nimeziona njia zake; nami nitamponya; nitamwongoza pia, nitamrudishia faraja zake, yeye na hao wanaomlilia.
19 Mimi nayaumba matunda ya midomo; Amani, amani, kwake yeye aliye mbali, na kwake yeye aliye karibu; asema BWANA; nami nitamponya.
Huruma ya Mungu;
Mungu alimwadhibu mwanadamu sababu ya dhambi, lakini anasema kwa huruma yake atamsamehe na kumponya. Pamoja na mwanadamu kuwa mkaidi, BWANA anasema hatakuwa na hasira! Anatangaza msamaha wa dhambi na uponyaji.
Kama tulivyosoma mstari wa (16) sisi hatuwezi kushindana na Mungu. Hivyo kwa tangazo hili la leo asubuhi, hima tudumu katika toba. Ukianzia nyuma kidogo, unaona kuwa Mungu anakaa na roho iliyotubu na kunyenyekea;
Isaya 57:15
15 Maana yeye aliye juu, aliyetukuka, akaaye milele; ambaye jina lake ni Mtakatifu; asema hivi; Nakaa mimi mahali palipoinuka, palipo patakatifu; tena pamoja na yeye aliye na roho iliyotubu na kunyenyekea, ili kuzifufua roho za wanyenyekevu, na kuifufua mioyo yao waliotubu.
Tubu dhambi zako.
Mungu wa huruma anasamehe na kutuponya.
Siku njema.
FRIDAY 24TH SEPTEMBER 2021, MORNING.
Isaiah 57:16-19 (NIV)
16 I will not accuse them forever,
nor will I always be angry,
for then they would faint away because of me—
the very people I have created.
17 I was enraged by their sinful greed;
I punished them, and hid my face in anger,
yet they kept on in their willful ways.
18 I have seen their ways, but I will heal them;
I will guide them and restore comfort to Israel’s mourners,
19 creating praise on their lips.
Peace, peace, to those far and near,”
says the Lord. “And I will heal them.”
God's mercy;
God punished man for his sin, but He says in His mercy He will forgive and heal him. Despite man's stubbornness, the LORD says he will not be angry! He proclaims forgiveness of sins and healing.
As we have read in verse (16) we cannot compete with God. So with this proclamation this morning, hurry and persevere in repentance. If you read the preceding verses, you see that God dwells with a repentant and humble spirit;
Isaiah 57:15
15 For this is what the high and exalted One says—
he who lives forever, whose name is holy:
“I live in a high and holy place,
but also with the one who is contrite and lowly in spirit,
to revive the spirit of the lowly
and to revive the heart of the contrite.
Repent of your sins.
The God of mercy forgives and heals us.
Good day.