Date: 
09-01-2025
Reading: 
Isaya 49:22-23

Hii ni Epifania 

Alhamisi asubuhi tarehe 09.01.2025

Isaya 49:22-23

22 Bwana MUNGU asema hivi, Tazama, nitawainulia mataifa mkono wangu, na kuwatwekea kabila za watu bendera yangu; nao wataleta wana wako vifuani mwao, na binti zako watachukuliwa mabegani mwao.

23 Na wafalme watakuwa baba zako za kulea, na malkia zao mama zako za kulea; watainama mbele yako kifudifudi, na kuramba mavumbi ya miguu yako; nawe utajua ya kuwa mimi ni Bwana, tena waningojeao hawatatahayarika.

Yesu ni nuru ya Ulimwengu;

Katika nyakati zote ambazo Israeli walipitia, Mungu hakuwahi kuwaacha. Sehemu tuliyosoma ni faraja ya Mungu kwao kwamba angewainulia mkono wake na kuwalinda. Ahadi ya Mungu ilikuwa ni kuwalinda na kuwatunza chini ya wafalme wao. Mungu aliwapa faraja hii walipokuwa uhamishoni, ambapo baadaye walikuja kutoka uhamishoni na kurudi kwenye nchi yao.

Ahadi ya Mungu ya kuwa na watu wake haikuishia hapo, maana ahadi zake ni za daima. Ahadi ya wokovu ilitimia pale Mungu alipotujia kama mwanadamu, kwa njia ya Yesu Kristo, akafa na kufufuka ili sisi tuokolewe. Kwa njia ya kifo na kufufuka kwake ametutoa gizani na kutuingiza nuruni, yaani ametuokoa na dhambi zetu. Mwamini sasa uokolewe. Amina

Alhamisi njema

Heri Buberwa