Date: 
05-03-2022
Reading: 
Yeremia 9:4-9

Jumamosi asubuhi tarehe 05.04.2022

Yeremia 9:4-9

4 Jihadharini, kila mtu na jirani yake, wala msimtumaini ndugu awaye yote; maana kila ndugu atachongea, na kila jirani atakwenda huko na huko na kusingizia.

5 Nao watadanganya kila mtu jirani yake, wala hawatasema kweli; wameuzoeza ulimi wao kusema uongo; hujidhoofisha ili kutenda uovu.

6 Makao yako ya katikati ya hadaa; kwa hadaa wanakataa kunijua mimi, asema Bwana.

7 Basi, kwa hiyo Bwana wa majeshi asema hivi, Tazama, nitawayeyusha na kuwajaribu; maana nisipotenda hivi, nitende nini kwa ajili ya binti ya watu wangu?

8 Ulimi wao ni mshale ufishao; husema maneno ya hadaa; mtu mmoja husema maneno ya amani na mwenzake kwa kinywa chake, lakini moyoni mwake humwotea.

9 Je! Nisiwapatilize kwa mambo hayo? Asema Bwana; na nafsi yangu je! Nisijilipize kisasi juu ya taifa la namna hii?

Kutubu na kurejea kwa Bwana;

Nabii Isaya analeta ujumbe kwa Taifa la Mungu, kuwa watu wamwangalie Mungu na siyo mwanadamu. Anawasihi watu kuwaepuka wenzao ambao siyo marafiki wa kudumu, maana waweza kuwahadaa wakati wowote. Bwana anaonya kulipiza kisasi kwa wote wategemeao wanadamu.

Ujumbe huu unatujia leo asubuhi ukituita kumcha na kumtegemea Bwana katika ulimwengu huu. Tunaitwa kuweka tumaini letu kwa Bwana, kwa kuchunguza njia zetu kama zinafaa mbele zake. Hatuwezi kumtumaini Bwana kama hatumfuati kwa ukamilifu, kwa msaada wa Roho Mtakatifu.

Tutubu na kurejea kwa Bwana.

Jumamosi njema.