
|
Vijana ambao walikuwa wanafunzi wa Sunday school, siku ya Jumamosi tarehe 21.11.2015 walibarikiwa rasmi kuanza kuhudhuria ibada ya watu wazima baada ya kufuzu mafunzo ya kipaimara waliyosoma kwa muda wa mika miwili, Msaidizi wa Askofu Chediel Lwiza ndie aliyeongoza ibada hiyo akishirikiana na na Mchungaji Kiongozi Charles Mzinga, na Mchungaji Prudence Chuwa. Mch. Lwiza alisema "Kuanzia leo mtakuwa mnaongozana na wazazi wenu na kuingia nao katika ibada ya watu wazima. Sasa, mnachotakiwa kiukifanya ni kujifunza neno la mungu na kulijua, mkikwama muonane na mchungaji ama waalimu wenu wa zamani wa sunday school, pia mnatakiwa kujiunga na kwaya mbalimbali ambazo zinahudumu hapa kanisani kwa sababu nyinyi sio watoto tena bali ni vijana" Ibada hiyo pia ilihudhuriwa na wazazi na walezi, walimu wa sunday school na washarika mbalimbali. Pia katika ibada hiyo kulikuwa na ubatizo wa mtoto mdogo mmoja na vijana wawili. Mambo yalikua kama ifuatavyo katika picha. |

Msaidizi wa Askofu Mch. Chediel Lwiza, Mch. Prudence Chuwa, Mch. Kiongozi Charles Mzinga na watoto wakiingia ibadani kwa
maadamano

Vijana waliohitimu mafunzo ya kipaimara wakifuatilia ibada

Vijana walioitimu mafunzo ya kipaimara wakifutilia ibada

Baadhi ya Wazazi na Washarika wakifuatilia ibada ya kipaimara kwa makini


Mchungaji Charles Mzinga akiendesha ibada ya kipaimara

Msaidizi wa Askofu Mch. Lwiza akiwabariki vijana



Kijana akikabidhiwa moja ya Biblia zilizopewa vijana wote waliobarikiwa


Mch. Chuwa akitoa mahubiri

Wachungaji wote 3 wakiendelea na ibada


Mch. Lwiza akibariki Divai ya Sakramenti ya meza ya Bwana

Mch. Mzinga Akibariki mkate wa Sakramenti
Parish worker Mama Urasa Akihudumu
Vijana washiriki Meza ya Bwana kwa mara ya kwanza

Kijana na Msharika wakishiriki

Watumishi wakishiriki

Vijana wakionyesha vyeti vyao vya kipaimara

Kikundi cha Matumbeta wakihudumu

Mwalimu Abisai akihudumu

Mwalimu wa ibada ya kiswahili Jane Mhina akiwa sambamba na Parish Worker Urasa wakifuatilia ibada ya kipaimara.

1Vijana 2 ambao pia waliobatizwa siku hiyo, wakiwa na wasimamizi wao wakisubiri kubatizwa

Kijana akibatizwa

1Msaidizi wa askofu Mch Chediel Lwiza akiwabariki wazazi wa mtoto aliyebatizwa.

1Kijana akitoa zawadi ya shukrani kwa Usharika kwa niaba ya vijana wote waliobarikiwa siku hiyo.

ÂÂÂ

Msaidizi wa Askofu na wachungaji wakifunga ibada.

Mch. Lwiza akitoa baraka.

Mchungaji Charles Mzinga akisema jambo kabla ya mwisho wa ibada.

ÂÂÂ Kikundi cha matarumbeta wakiongoza ibada kutoka nje kwa maadamano

1Mchungaji Prudence Chuwa akimpongeza kijana aliyepata kipaimara

1Msaidizi wa askofu akiwa ameambatana na Mchungaji Prudence Chuwa akiwa katika picha ya pamoja na vijana waliopata kipaimara
sambamba na wazazi wao.

1Mchungaji Charles Mzinga akimpa mkono wa amani Mchungaji Prundece Chuwa baada ya ibada kumalizika.

Vijana waliobarikiwa wakiwa katika picha ya pamoja.

Wana Matarumbeta wakiwa nje ya kanisa kufunga ibada.

ÂÂÂ 
Mch. Mzinga akiteta jambo na mpiga tarumbeta.
(Picha na habari na Jane Mhina)
