Date:
21-01-2026
Reading:
Marko 2:1-5
Hii ni Epifania
Jumatano asubuhi tarehe 21.01.2026
Marko 2:1-5
1 Akaingia Kapernaumu tena, baada ya siku kadha wa kadha, ikasikiwa ya kwamba yumo nyumbani.
2 Wakakusanyika watu wengi, isibaki nafasi hata mlangoni; akawa akisema nao neno lake.
3 Wakaja watu wakimletea mtu mwenye kupooza, anachukuliwa na watu wanne.
4 Na walipokuwa hawawezi kumkaribia kwa sababu ya makutano, waliitoboa dari pale alipokuwapo; na wakiisha kuivunja wakalitelemsha godoro alilolilalia yule mwenye kupooza.
5 Naye Yesu, alipoiona imani yao, akamwambia yule mwenye kupooza, Mwanangu, umesamehewa dhambi zako.
Nyumba zetu hubarikiwa na Mungu;
Yesu alikuwa ameingia Kapernaumu, akawa amekaa na watu wengi nyumbani isiwepo nafasi hata mlangoni. Wapo ndugu waliokuwa na ndugu yao mgonjwa aliyepooza, walimleta kwa Yesu amponye. Walipoona hakuna nafasi, walitoboa dari wakamteremsha mgonjwa pale alipokuwapo Yesu. Yesu alipoona imani, akamtangazia msamaha wa dhambi yule aliyepooza.
Ukiendelea kusoma unaona Yesu akimwambia aliyepooza kujitwika godoro na kuondoka;
Marko 2:11-12
11 Nakuambia, Ondoka, ujitwike godoro lako uende nyumbani kwako. 12 Mara akaondoka, akajitwika godoro lake, akatoka mbele yao wote; hata wakastaajabu wote, wakamtukuza Mungu, wakisema, Namna hii hatujapata kuiona kamwe.Wale ndugu waliokuwa na mgonjwa walikuwa na imani katika Yesu Kristo, ndiyo maana alipoiona imani yao akamponya mgonjwa wao. Nasi tukimwamini Yesu anabariki nyumba zetu. Amina
Jumatano njema
Heri Buberwa Nteboya
0784 968650
