Date: 
19-01-2026
Reading: 
Mwanzo 20:17-18

Hii ni Epifania 

Jumatatu asubuhi tarehe 19.01.2026

Mwanzo 20:17-18

17 Ibrahimu akamwomba Mungu, Mungu akamponya Abimeleki, na mkewe, na wajakazi wake, nao wakazaa wana.

18 Maana Bwana alikuwa ameyafunga matumbo ya watu wa nyumbani mwa Abimeleki, wasizae, kwa ajili ya Sara mkewe Ibrahimu. 

Nyumba zetu hubarikiwa na Mungu;

Asubuhi ya leo tunamsoma Ibrahimu akiwa katika nchi ya Kusini, akitembea katika Gerari. Alikuwa na Sara mke wake, lakini alimtambulisha kama ndugu yake maana aliona kuwa watu wa nchi ile hawakuwa na hofu ya Mungu. Abimeleki alimtwaa Sara, lakini Mungu akamzuia katika ndoto asimtwae Sara maana ni mke wa Ibrahimu. Abimeleki akawa mtii na kumrudisha Sara kwa Ibrahimu.

Ndipo somo linamuonesha Ibrahimu akimuomba Mungu amponye Abimeleki, mkewe na wajakazi wake wapate watoto. Mungu alisikia sala ya Ibrahimu, Abimeleki akapona, mkewe na wajakazi wakazaa wana. Nyumba ya Abimeleki ilibarikiwa kwa sababu alimtii Mungu. Nasi tukimwamini Yesu anabariki nyumba zetu. Amina

Uwe na wiki njema

 

Heri Buberwa