Date:
19-12-2025
Reading:
Luka 13:18-20
Hii ni Advent
Ijumaa asubuhi tarehe 19.12.2025
Luka 3:18-20
18 Basi, kwa maonyo mengine mengi aliwahubiri watu.
19 Lakini mfalme Herode alipokaripiwa na yeye kwa ajili ya Herodia, mke wa nduguye, na maovu yote aliyoyafanya Herode,
20 aliongeza na hili juu ya yote, alimfunga Yohana gerezani.
Itengenezeni njia ya Bwana;
Yohana alitangaza kuja kwa Yesu Kristo, yaani alimtangulia Yesu. Alitangaza na kuhubiri kwamba watu wasafishe mioyo yao wakijiandaa kumpokea Yesu. Alihubiri, alifundisha, mkazo mkubwa ukiwa ni njia ya ufalme wa Mungu kwa kujiandaa kumpokea Yesu. Wakati anahubiri hivi, alikuwa nyikani akila asali ya mwitu na nzige
Sasa wakati akitimiza utume huo, Yohana alimkaripia Herode aliyekuwa amemuoa Herodia mke wa Filipo nduguye. Alimwambia Herode kwamba ndoa yake ilikuwa batili! Ilimgharimu Yohana kukatwa kichwa! Katika kumtangaza Kristo Yohana alisimamia ukweli hata uliogharimu maisha yake. Changamoto tunazopitia zisitutoe kwa Kristo, bali tuimarike katika imani tukingojea kurudi kwake. Amina
Siku njema
Heri Buberwa Nteboya
0784 968650
