Date: 
16-12-2025
Reading: 
Isaya 40:6-9

Hii ni Advent 

Jumanne asubuhi tarehe 16.12.2025

Isaya 40:6-9

6 Sikiliza, ni sauti ya mtu asemaye, Lia! Nikasema, Nilie nini? Wote wenye mwili ni majani, Na wema wake wote ni kama ua la kondeni;

7 Majani yakauka, ua lanyauka; Kwa sababu pumzi ya Bwana yapita juu yake. Yakini watu hawa ni majani.

8 Majani yakauka, ua lanyauka; Bali neno la Mungu wetu litasimama milele.

9 Wewe uuhubiriye Sayuni habari njema, Panda juu ya mlima mrefu; Wewe uuhubiriye Yerusalemu habari njema, Paza sauti kwa nguvu; Paza sauti yako, usiogope; Iambie miji ya Yuda, Tazameni, Mungu wenu.

Itengenezeni njia ya Bwana;

Juzi Jumapili tulisikia tafakari iliyotuonesha Mungu akiwafariji watu wake kwa ahadi ya kuwakomboa (Isaya 40:1-5). Somo la asubuhi ya leo ni mwendelezo wa ahadi hiyo, ikiwa ni sauti ya mtu asemaye lia, na mwingine anauliza alie nini? Hii inaonesha faraja ya Mungu kwa wenye huzuni, kwamba huzuni yao itageuka furaha. Yaani Israeli wanapewa ahadi ya kukombolewa. Ukiendelea kusoma unaona Isaya akikazia juu ya ukombozi wao;

Isaya 40:10-11

10 Tazameni, Bwana Mungu atakuja kama shujaa, Na mkono wake ndio utakaomtawalia; Tazameni, thawabu yake i pamoja naye, Na ijara yake i mbele zake.
11 Atalilisha kundi lake kama mchungaji, Atawakusanya wana-kondoo mikononi mwake; Na kuwachukua kifuani mwake, Nao wanyonyeshao atawaongoza polepole.

Anatabiriwa Bwana ambaye atakuja kama shujaa, ambaye atalilisha kundi lake kama Mchungaji. Atawakusanya kondoo mikononi mwake na kuwaongoza katika njia sahihi. Huyu ni Yesu Kristo aliyekuja duniani kuokoa wanadamu, na atarudi tena kulichukua Kanisa. Jiandae kumpokea. Amina

Siku njema

 

Heri Buberwa Nteboya 

0784 968650 

bernardina.nyamichwo@gmail.com