Date: 
18-12-2023
Reading: 
Yohana 1:15-18

Hii ni Advent 

Jumatatu asubuhi tarehe 18.12.2023

Yohana 1:15-18

15 Yohana alimshuhudia, akapaza sauti yake akasema, Huyu ndiye niliyenena habari zake ya kwamba, Ajaye nyuma yangu amekuwa mbele yangu; kwa maana alikuwa kabla yangu.

16 Kwa kuwa katika utimilifu wake sisi sote tulipokea, na neema juu ya neema.

17 Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa; neema na kweli zilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo.

18 Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote; Mungu Mwana pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyemfunua.

Itengenezeni njia ya Bwana;

Injili ya Yohana inaanza kwa kumtaja Yesu Kristo kama neno aliyekuwa kwa Mungu, akaja kwetu na utukufu wake ukaonekana. Huyu ndiye aliyeshuhudiwa na Yohana kama Mwokozi anayekuja kuokoa ulimwengu akiwaita watu kuandaa mioyo yao kumpokea. Yesu anashuhudiwa kuileta neema iokoayo wanadamu, tofauti na Musa aliyekuja na torati.

Neema ya Kristo ingalipo hata sasa, ikitualika kuandaa mioyo yetu kumpokea Kristo. Kristo akae mioyoni mwetu daima, na kwa njia hii tutawezeshwa kutenda yatupasayo katika maisha yetu, tayari kumpokea akirudi mara ya pili na kuurithi uzima wa milele. Amina.

Tunakutakia wiki njema.

 

Heri Buberwa