Hii ni Pasaka
Jumanne asubuhi tarehe 02.05.2023
Yohana 16:1-14
1 Maneno hayo nimewaambia, msije mkachukizwa.
2 Watawatenga na masinagogi; naam, saa yaja atakapodhania kila mtu awauaye ya kuwa anamtolea Mungu ibada.
3 Na hayo watawatenda kwa sababu hawakumjua Baba wala mimi.
4 Lakini nimewaambia hayo, ili makusudi saa ile itakapokuja myakumbuke ya kuwa mimi naliwaambia. Sikuwaambia hayo tangu mwanzo, kwa sababu nalikuwapo pamoja nanyi.
5 Lakini sasa mimi naenda zangu kwake yeye aliyenipeleka, wala hakuna mmoja wenu aniulizaye, Unakwendapi?
6 Ila kwa sababu nimewaambia hayo huzuni imejaa mioyoni mwenu.
7 Lakini mimi nawaambia iliyo kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke, kwa maana mimi nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu.
8 Naye akiisha kuja, huyo atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu.
9 Kwa habari ya dhambi, kwa sababu hawaniamini mimi;
10 kwa habari ya haki, kwa sababu mimi naenda zangu kwa Baba, wala hamnioni tena;
11 kwa habari ya hukumu, kwa sababu yule mkuu wa ulimwengu huu amekwisha kuhukumiwa.
12 Hata bado nikali ninayo mengi ya kuwaambia, lakini hamwezi kuyastahimili hivi sasa.
13 Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.
14 Yeye atanitukuza mimi, kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari.
Maisha mapya ndani ya Yesu;
Yesu alifundisha akiwaambia wanafunzi wake kuwa wasifadhaike kwa kuwa kwa Baba yake kuna makao mengi. Akawaambia yeye ni mzabibu, akawausia kuwa na upendo kati yao. Lakini ahadi kubwa zaidi akawaambia kuwa ataondoka, na atawaachia Msaidizi, Roho Mtakatifu (sura 14 na 15)
Katikati ya yote hayo, ndipo katika sura ya 16 anawaambia watachukizwa kwa ajili yake, watawatenga na kuwatesa. Lakini katika yote hayo Yesu anahitimisha kwa kusema;
Yohana 16:33 Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.Mazingira tunayoishi na kazi zetu visitufanye kumuacha Yesu. Tuwe na imani katika yeye aliyeshinda Ulimwengu ili maisha yetu yawe mapya siku zote. Siku njema.
Heri Buberwa