Date: 
15-07-2022
Reading: 
Isaiah 46:3-4

Ijumaa asubuhi tarehe 15.07.2022

Isaya 46:3-4

[3]Nisikilizeni, enyi wa nyumba ya Yakobo, ninyi mlio mabaki ya nyumba ya Israeli, mliochukuliwa nami tangu tumboni, mlioinuliwa tangu mimbani;

[4]na hata uzee wenu mimi ndiye, na hata wakati wenu wa mvi nitawachukueni; nimefanya, nami nitachukua; naam, nitachukua na kuokoa.

Mungu ni mwingi wa huruma na haki;

Mungu ananena na Israeli kupitia kwa Nabii Isaya kwamba yeye ndiye Mungu wa Yakobo astahiliye kusikilizwa. Anajidhihirisha kama Mungu wao, aliyekuwa nao tangu kale, aliye nao, na atakaye kuwa nao. Ukiendelea kusoma mstari wa tano unaona yeye hafananishwi na mtu wala kitu chochote. Yeye ndiye Bwana.

Yesu Kristo ndiye Mwokozi wa ulimwengu aliyekuwepo, aliyepo na atakayekuwepo. Imeandikwa;

Waebrania 13:8
[8]Yesu Kristo ni yeye yule, jana na leo na hata milele.

Kumbe usalama wetu ni kumwamini Mungu aliyepo milele yote ili tuurithi uzima wa milele.

Ijumaa njema.