Date: 
20-09-2017
Reading: 
Acts 9:36-43 NIV ( Matendo 9:36-43)

WEDNESDAY 20TH SEPTEMBER 2017 MORNING                       

Acts 9:36-43 New International Version (NIV)

36 In Joppa there was a disciple named Tabitha (in Greek her name is Dorcas); she was always doing good and helping the poor. 37 About that time she became sick and died, and her body was washed and placed in an upstairs room. 38 Lydda was near Joppa; so when the disciples heard that Peter was in Lydda, they sent two men to him and urged him, “Please come at once!”

39 Peter went with them, and when he arrived he was taken upstairs to the room. All the widows stood around him, crying and showing him the robes and other clothing that Dorcas had made while she was still with them.

40 Peter sent them all out of the room; then he got down on his knees and prayed. Turning toward the dead woman, he said, “Tabitha, get up. "She opened her eyes, and seeing Peter she sat up. 41 He took her by the hand and helped her to her feet. Then he called for the believers, especially the widows, and presented her to them alive. 42 This became known all over Joppa, and many people believed in the Lord. 43 Peter stayed in Joppa for some time with a tanner named Simon.

Dorcas was much loved for her kindness and practical help to those in need. She used the talents which God gave her to serve others.  There was much grief when she died. But Peter by the power of God was able to work a miracle and bring her back to life.

What legacy are you building? Are you using your talents and abilities to serve God and to help other people? 

JUMATANO TAREHE 20 SEPTEMBA 2017 ASUBUHI              

MATENDO  9:36-43

36 Na mwanafunzi mmoja alikuwako Yafa, jina lake Tabitha, tafsiri yake ni Dorkasi (yaani paa); mwanamke huyu alikuwa amejaa matendo mema na sadaka alizozitoa. 
37 Ikawa siku zile akaugua, akafa; hata walipokwisha kumwosha, wakamweka orofani. 
38 Na kwa kuwa mji wa Lida ulikuwa karibu na Yafa, nao wanafunzi wamesikia ya kwamba Petro yuko huko, wakatuma watu wawili kwake, kumsihi na kusema, Usikawie kuja kwetu. 
39 Petro akaondoka akafuatana nao. Alipofika, wakampeleka juu orofani wajane wote wakasimama karibu naye, wakilia na kumwonyesha zile kanzu na nguo alizozishona Dorkasi wakati ule alipokuwa pamoja nao. 
40 Petro akawatoa nje wote, akapiga magoti, akaomba, kisha akaelekea yule maiti, akanena, Tabitha, ondoka. Naye akafumbua macho yake, na alipomwona Petro akajiinua, akaketi. 
41 Akampa mkono, akamwinua; hata akiisha kuwaita wale watakatifu na wajane akamweka mbele yao, hali yu hai. 
42 Ikajulikana katika mji mzima wa Yafa; watu wengi wakamwamini Bwana. 
43 Basi Petro akakaa siku kadha wa kadha huko Yafa, nyumbani mwa mtu mmoja, jina lake Simoni, mtengenezaji wa ngozi.

Tabitha alipendwa sana na watu hasa wajane kwa jinsi alivyowasaidia. Walisikitika sana alipofariki. Lakini Petro kwa nguvu ya Mungu aliweza kutenda muujiza na kumfufua.

Wewe je! Utaacha urithi gani? Watu watakukumbuka kwa kitu gani? Tumia karama na vipawa ulivyopewa na Mungu kufanya kazi yake hapa duniani na kubariki binadamu wenzako.