Date: 
17-12-2022
Reading: 
Luka 7:18-23

Hii ni Advent 

Jumamosi asubuhi tarehe 17.11.2022

Luka 7:18-23

[18]Wanafunzi wa Yohana wakamletea habari za hayo yote.

[19]Ndipo Yohana alipowaita wawili katika wanafunzi wake, akawatuma kwa Yesu akiuliza, Wewe ndiwe yule ajaye, au tumtazamie mwingine?

[20]Nao walipofika kwake, walisema, Yohana Mbatizaji ametutuma kwako, akisema, Wewe ndiwe yule ajaye, au tumtazamie mwingine?

[21]Na saa ile ile aliwaponya wengi magonjwa yao, na misiba, na pepo wabaya; na vipofu wengi aliwakirimia kuona.

[22]Ndipo alipojibu, akawaambia, Nendeni mkamweleze Yohana hayo mliyoyaona na kuyasikia; vipofu wanapata kuona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakasika, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, maskini wanahubiriwa habari njema.

[23]Naye heri mtu ye yote asiyechukizwa nami.

Bwana anawafariji watu wake;

Yohana akiwa gerezani aliletewa habari za Yesu na wanafunzi wake (Yohana). Akawatuma wakamuulize Yesu kama yeye ndiye Mesiya au waendelee kumngojea mwingine? Yesu akawatuma wanafunzi wa Yohana akijibu kuwa wakamwambie habari za huduma yake na yote yaliyotendeka.

Yesu alikuwa anadhihirisha kwa Yohana kwamba yeye ndiye Mesiya, aliyetabiriwa akaja kwa ajili ya kuwaokoa wanadamu na dhambi zao. Yesu alisema wakati ule akimjibu Yohana, lakini hata leo ndiye Mwokozi wa ulimwengu. Atarudi tena kuwafufua walio hai na wafu, tayari kwa uzima wa milele kwa wote waliompokea, wakamwamini na kumfuata. Uwe na Jumamosi njema.

Amina.