Date: 
19-03-2022
Reading: 
2 Samweli 4:4-12

Hii ni Kwaresma 

Jumamosi asubuhi tarehe 19.03.2022

2 Samweli 4:4-12

4 Naye Yonathani, mwana wa Sauli alikuwa na mwana aliyekuwa na kilema cha miguu. Alikuwa amepata miaka mitano, habari za Sauli na Yonathani zilipofika Yezreeli, na yaya wake akamchukua akakimbia ikawa, alipokimbia kwa haraka, huyo mtoto akaanguka, akawa kilema. Na jina lake aliitwa Mefiboshethi.

5 Na wale wana wa Rimoni, Mbeerothi, Rekabu na Baana, wakaenda wakafika nyumbani kwa Ishboshethi, wakati wa hari ya mchana, alipokuwa akipumzika adhuhuri.

6 Wakafikia kati ya nyumba, kana kwamba wanataka kuchukua ngano, wakampiga mkuki wa tumbo; kisha Rekabu na Baana nduguye wakakimbia.

7 Basi walipoingia katika ile nyumba, alipokuwa amelala kitandani mwake, katika chumba chake cha kulala, wakampiga, wakamwua, wakamkata kichwa, wakachukua kichwa chake, wakaenda zao kwa njia ya Araba usiku kucha.

8 Wakamletea Daudi kichwa cha Ishboshethi huko Hebroni, wakamwambia mfalme, Tazama, hiki ni kichwa cha Ishboshethi, mwana wa Sauli, adui yako, aliyekutafuta roho yako; Bwana amemlipia kisasi bwana wangu mfalme hivi leo, juu ya Sauli, na juu ya wazao wake.

9 Naye Daudi akawajibu Rekabu na Baana, nduguye, wana wa Rimoni, Mbeerothi, akawaambia, Aishivyo Bwana, aliyenihifadhi roho yangu katika shida zote,

10 mtu mmoja aliponiambia, akasema, Tazama, Sauli amekufa, akidhani ya kuwa ameleta habari njema, nalimshika, nikamwua, huko Siklagi, ndio ujira niliompa kwa habari zake.

11 Basi, iwapo watu waovu wamemwua mtu mwenye haki kitandani mwake, je! Sasa nisitake zaidi damu yake mikononi mwenu, na kuwaondoa ninyi katika nchi?

12 Ndipo Daudi akawaagiza vijana wake, wakawaua, wakawakata mikono na miguu, wakawatundika kando ya ziwa katika Hebroni. Nao wakakitwaa kichwa cha Ishboshethi wakakizika katika kaburi la Abneri huko Hebroni.

Tupinge ukatili;

Rekabu na Baana walimuua kwa kumkata kichwa Ishboshethi mwana wa Sauli, aliyekuwa adui yake Daudi, wakamletea habari Daidi. Daudi hakuwaunga mkono, aliamuru nao wauawe! (12)

Pale tunapoamua kuwaumiza wengine kwa sababu wametuudhi tunakuwa hatuko sawa. Usimwadhibu aliyekosea kwa kukosea. Yaani maamuzi juu ya wanaotukosea yawe yenye utukufu wa Mungu, yaani msamaha katika Kristo Yesu. 

Uwe na Jumamosi njema.