Date: 
09-08-2019
Reading: 
Romans 4:1-8 (Warumi 4:1-8)

FRIDAY 9TH AUGUST 2019 MORNING                                      

Romans 4:1-8 New International Version (NIV)

Abraham Justified by Faith

What then shall we say that Abraham, our forefather according to the flesh, discovered in this matter? If, in fact, Abraham was justified by works, he had something to boast about—but not before God. What does Scripture say? “Abraham believed God, and it was credited to him as righteousness.”[a]

Now to the one who works, wages are not credited as a gift but as an obligation. However, to the one who does not work but trusts God who justifies the ungodly, their faith is credited as righteousness. David says the same thing when he speaks of the blessedness of the one to whom God credits righteousness apart from works:

“Blessed are those
    whose transgressions are forgiven,
    whose sins are covered.
Blessed is the one
    whose sin the Lord will never count against them.”[
b]

Footnotes:

  1. Romans 4:3 Gen. 15:6; also in verse 22
  2. Romans 4:8 Psalm 32:1,2

The Apostle Paul reminds the Roman Christians and us too that we cannot earn our salvation. Salvation is a gift of God which we receive by Faith in Christ. Jesus died to pay the penalty for our sins so we need to keep repenting our sins and trusting in Jesus Christ.

Let us do our best to obey God but we can never boast that we have earned our salvation.


IJUMAA TAREHE 9 AGOSTI 2019 ASUBUHI                           

RUMI 4:1-8

1 Basi, tusemeje juu ya Ibrahimu, baba yetu kwa jinsi ya mwili? 
Kwa maana ikiwa Ibrahimu alihesabiwa haki kwa ajili ya matendo yake, analo la kujisifia; lakini si mbele za Mungu. 
Maana maandiko yasemaje? Ibrahimu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa haki. 
Lakini kwa mtu afanyaye kazi, ujira wake hauhesabiwi kuwa ni neema, bali kuwa ni deni. 
Lakini kwa mtu asiyefanya kazi, bali anamwamini yeye ambaye amhesabia haki asiyekuwa mtauwa, imani yake mtu huyo imehesabiwa kuwa haki. 
Kama vile Daudi aunenavyo uheri wake mtu yule ambaye Mungu amhesabia kuwa na haki pasipo matendo, 
Heri waliosamehewa makosa yao, Na waliositiriwa dhambi zao. 
Heri mtu yule ambaye Bwana hamhesabii dhambi. 
 

Mtume Paulo anawakumbusha Wakristo kule Rumi, na anatukumbusha sisi pia, kwamba hatuwezi kupata wokovu kwa nguvu zetu na kazi zetu. Wokovu ni zawadi kutoka kwa Mungu. Tunapaswa kupokea zawadi hii kwa njia ya Imani katika Yesu Kristo. Yesu alilipa deni la dambi zetu kwa kifo chake msalabani. Tuendelee kutubu dhambi zetu na kumwamini na kumtegemea Yesu Kristo.

Ni vema kujitahidi kutii amri za Mungu lakini hatuwezi kudai ni matendo yetu ndio yametuokoa.