DAYOSISI YA MASHARIKI NA PWANI
MATANGAZO YA USHARIKA YA TAREHE 3 Mei, 2026
SIKU YA BWANA YA 4 BAADA YA PASAKA
KANTATE DOMINO - MWIMBIENI BWANA WIMBO MPYA. NENO LINALOTUONGOZA NI:
“NJOONI TUMSIFU MUNGU WETU”
1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia na cheti.
3. Matoleo ya Tarehe 26/04/2026
Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.
NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:
- 0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT
Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL
4. Mahudhurio ya ibada za tarehe 19/04/2026 ni Washarika 704
5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Ibada ya asubuhi saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada ya mchana saa 7.00 mchana. Ijumaa saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front Cathedral.
6. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=.
7. Leo tarehe 03/05/2026 tutamtolea Mungu fungu la Kumi. Washarika karibuni.
8. Kwaya Kuu ya Usharika leo wanashiriki ibada Kanisa Kuu Bungo Morogoro. Washarika tuwaombee.
9. Shukrani: Jumapili ijayo tarehe 10/05/2026 katika ibada ya kwanza
- Mama Theudas Msangi atamshukuru Mungu kwa kumbukumbu yake ya kuzaliwa kufikisha miaka 82 tarehe 08.05., Matendo makuu aliyomtendea, kumponya magonjwa mazito na mitihani migumu hata kufikisha umri huu akiwa na afya nzuri.
Neno: Zaburi 71:4-9 , Wimbo: TMW 295
10. NDOA. NDOA WASHARIKA
KWA MARA YA TATU TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 09/05/2026
SAA 9.00 ALASIRI
Bw. Fredrick Leonard Kowero na Bi. Anitha Frank Saria.
Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu.
11. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA
- Mjini kati: Kwa watashiriki hapa Kanisani saa 1.00 asubuhi
- Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bwana na Bibi Frank Korassa.
- Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach: Kwa Mama Theudas Msangi
12. Kwa habari na taarifa nyingine, tembelea tovuti yetu ya Azania front. org, pia tupo Facebook na Instagram.
-
Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la Pili
