Date: 
03-08-2019
Reading: 
Mathew 22:34-40

SATURDAY 3RD AUGUST 2019 MORNING                                       
Matthew 22:34-40 New International Version (NIV)
The Greatest Commandment
34 Hearing that Jesus had silenced the Sadducees, the Pharisees got together. 35 One of them, an expert in the law, tested him with this question: 36 “Teacher, which is the greatest commandment in the Law?”
37 Jesus replied: “‘Love the Lord your God with all your heart and with all your soul and with all your mind.’[a] 38 This is the first and greatest commandment. 39 And the second is like it: ‘Love your neighbor as yourself.’[b] 40 All the Law and the Prophets hang on these two commandments.”
Footnotes:
Matthew 22:37 Deut. 6:5
Matthew 22:39 Lev. 19:18


Jesus faced many challenging questions from the Jewish Religious leaders, the Sadducees and the Pharisees. They were not genuinely seeking answers to their questions but they were trying to trap and discredit Jesus.  But they never succeeded. Jesus always had the perfect answer for them. 
Jesus shows here that all the commandments are important and they can be summed up by loving God and loving other people. This should still be our aim today.



JUMAMOSI TAREHE 3 AGOSTI 2019 ASUBUHI                            
Mathayo 22:34-40
34 Na Mafarisayo waliposikia ya kwamba amewafumba kinywa wale Masadukayo, walifanya shauri pamoja. 
35 Mmoja wao, mwana-sheria, akamwuliza, akimjaribu; 
36 Mwalimu, katika torati ni amri ipi iliyo kuu? 
37 Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote. 
38 Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza. 
39 Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. 
40 Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii. 

Viongozi wa dini wa Kiyahudu, Masadukayo na Mafarisayo, mara kwa mara waliuliza Yesu maswali. Lengo lao ilikuwa siyo kupata majibu sahihi bali kumwangusha na kumwaibisha Yesu. Lakini hawakufanyikiwa. Yesu alikuwa na jibu kamili kila wakati.
Yesu hapa anaonyesha kwamba amri zote 10 ni muhimu na zinawezakujumlishwa kwa kupenda Mungu na kupenda binadamu mwenzako.  Hadi leo inapaswa kuwa lengo yetu kufanya hivi.