MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 02 DESEMBA, 2017

SOMO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI BWANA ANALIJIA KANISA LAKE

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.

2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia na cheti. Kama kuna wageni walioshiriki nasi mara ya kwanza wasimame ili tuweze kuwakaribisha.

3. Leo tarehe 03.11.2017 saa 10.00 jioni hapa Usharikani kutakuwa na faragha ya maombi ya Kamati ya Misioni na uinjilisti, wajumbe wote wa kamati wanaarifiwa ili wafike na tuanze kwa muda. Aidha wajumbe wa kamati nyingine za baraza wanakaribishwa katika maombi hayo ikiwa ni pamoja na wajumbe wa baraza la Wazee na msharika yeyote atayesukumwa kuungana na Kamati ya Misioni na Uinjilisti katika maombi hayo.  Njooni tumlilie Mungu juu ya Usharika wetu na familia zetu. Pia siku ya Alhamisi tarehe 07/11/2017 kutakuwa na kipindi cha maombi na maombezi. Kipindi hicho kitaongozwa na Mwinjilisti Emmanuel Franki toka KKKT Usharika wa Tumbi.  Wenye mahitaji wataombewa.

4. Washarika mnaombwa kujaza fomu kwa ajili ya utaratibu mpya wa namba za Bahasha. Bado washarika wachache hawajarudisha fomu hizo.  Unapojaza fomu hii usisahau kujaza namba yako unayotumia sasa. Zoezi hili litaendelea hadi tarehe 10.12.2017.  Baada ya tarehe hiyo namba mpya zitatolewa.

5. Ijumaa ijayo tarehe 08/12/2017 saa 11.00 jioni kutakuwa na kikao cha Kamati ya utendaji ya Baraza la Wazee. Kamati mbalimbali zinaombwa kukutana kwa ajili ya maandalizi ya kikao hicho.

6. Leo Kwaya ya Wanawake wanahudumu Usharika wa Hananasifu.  Washarika tuwaombee.

7. Vikundi vyote vya usharika vinaombwa kuwasilisha bajeti zao.  Mwisho wa kupokea Bajeti ni tarehe 07/12/2017. Aidha kutakuwa na kikao cha Wenyeviti wa vikundi vyote wakutana na Kamati ya Misioni na Uinjilisti Siku ya jumanne tarehe 5/12/2017 saa 11.00 jioni kwa ajili ya kuanda  ratiba ya Tamasha pamoja na mambo mengine.

8. Washarika walioahidi na waliochukua vitu kwa mnada siku ya mavuno pamoja na Harambee ya Kiharaka wanaombwa kukamilisha ahadi zao ofisi ya wahasibu.

9. Tarehe 24/12/2017 kutakuwa na ubatizo wa watoto na kurudi kundini. Hakutakuwa na ubatizo tarehe 26/12/2017 kama ilivyozoeleka. Siku hiyo kutakuwa na Kipaimara Dayosisi nzima ambayo itafanyika hapa Kanisa Kuu Azania Front.

10. Jumapili ijayo tarehe 10/12/2017 katika ibada ya pili Familia ya Fuya G. Kimbita watamshukuru Mungu kwa Mambo mema aliyowatendea.

Neno: Zaburi 138:1-3, Wimbo: TMW 257

 

11. NDOA

HAKUNA NDOA ZA WASHARIKA

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo Karibu na duka letu la vitabu.

 

12. Ibada za Nyumba kwa Nyumba

  • Upanga: Watatangaziana
  • Kinondoni: Kwa Bwana na Bibi Jackson Kaale
  • Ilala/Chang’ombe/Mivinjeni: Watatangaziana
  • Kawe/Mikocheni/Mbezi Beach: Kwa Mama Chamungwana
  • Oysterbay/Masaki: Kwa Bwana na Bibi Raphael Mollel
  • Kijitonyama/Sinza/Mwenge/Makumbusho/Ubungo: kwa Bwana na Bibi Simon Jengo
  • Mjini kati: Kwa Bibi Lydia Ngwale
  • Wazo/tegeta/Kunduchi/BahariBeach/Ununio: Kwa Prof. na Bibi Judica Lawson
  • Tabata: Kwa Bwana na Bibi Mwakasege

Zamu: Zamu za wazee ni Kwanza.

Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki.