Date: 
17-03-2017
Reading: 
Genesis 27:41-45 (NIV)

FRIDAY 17TH MARCH 2017 MORNING                                 

Genesis 27:41-45 New International Version (NIV)

41 Esau held a grudge against Jacob because of the blessing his father had given him. He said to himself, “The days of mourning for my father are near; then I will kill my brother Jacob.”

42 When Rebekah was told what her older son Esau had said, she sent for her younger son Jacob and said to him, “Your brother Esau is planning to avenge himself by killing you. 43 Now then, my son, do what I say: Flee at once to my brother Laban in Harran. 44 Stay with him for a while until your brother’s fury subsides. 45 When your brother is no longer angry with you and forgets what you did to him, I’ll send word for you to come back from there. Why should I lose both of you in one day?”

There was a strong rivalry between these twin brothers Esau and Jacob. Jacob had cheated Esau out of his birthright as first born. This caused Esau to hate and to want to kill Jacob.

Let us pray for love and harmony in our families and do what we can to reconcile any disputes in our own family. God desires that we should love one another.

IJUMAA TAREHE 17 MACHI 2017 ASUBUHI                          

MWANZO  27:41-45

41 Esau akamchukia Yakobo kwa ajili ya ule mbaraka babaye aliombarikia. Esau akasema moyoni mwake, Siku za kumlilia baba yangu zinakaribia, ndipo nitakapomwua ndugu yangu Yakobo. 
42 Rebeka akaarifiwa maneno ya Esau, mwanawe mkubwa. Akapeleka mtu kumwita Yakobo, mwanawe mdogo, akamwambia, Tazama, katika habari zako Esau, ndugu yako, anajifariji moyo wake, maana anakusudia kukuua. 
43 Na sasa, mwanangu, sikia sauti yangu, uondoke, ukimbilie kwa Labani, ndugu yangu huko Harani; 
44 ukae kwake siku chache, hata ghadhabu ya ndugu yako igeuke; 
45 hata ikuondokee ghadhabu ya ndugu yako, akasahau uliyomtenda. Ndipo nitakapopeleka watu kukuchukua kutoka huko. Kwa nini nifiwe nanyi nyote wawili siku moja? 
 

Kulikuwa na chuki na ushindani kati ya Esau na pacha wake Yakobo. Yakobo alimdhulumu Esau na kuchukua haki yake kama mzaliwa wa kwanza. Hali hii ilimsababisha chuki ndani yake na alitaka kumuua mdogo wake.

Mara kwa mara kuna ugomvi katika familia zetu. Tujitahidi kuleta amani na mapatano katika familia zetu. Tumwombe Mungu upendo itawale.