Date: 
02-06-2017
Reading: 
DANIEL 9:4-9

FRIDAY 2ND JUNE 2017                              

Daniel 9:4-9 New International Version (NIV)

I prayed to the Lord my God and confessed:

“Lord, the great and awesome God, who keeps his covenant of love with those who love him and keep his commandments, we have sinned and done wrong. We have been wicked and have rebelled; we have turned away from your commands and laws. We have not listened to your servants the prophets, who spoke in your name to our kings, our princes and our ancestors, and to all the people of the land.

“Lord, you are righteous, but this day we are covered with shame—the people of Judah and the inhabitants of Jerusalem and all Israel, both near and far, in all the countries where you have scattered us because of our unfaithfulness to you. We and our kings, our princes and our ancestors are covered with shame, Lord, because we have sinned against you. The Lord our God is merciful and forgiving, even though we have rebelled against him;

 

This week and last week we have been focusing on prayer.

The Bible gives much advice about how we should pray to God. The Bible also gives us several examples of prayers. Above is one of Daniel’s prayers. We can study his prayer and learn something which we can apply in our own prayers.

Daniel praises God for His greatness and His goodness.  Daniel also acknowledges the sins of the people.

It is good to begin our prayers with praise to God and confessing our sins to God before we ask God for help with our needs. 

 

IJUMAA TAREHE 2 JUNI 2017 ASUBUHI                                  

DANIELI 9:4-9

 

4 Nikamwomba Bwana, Mungu wangu, nikaungama, nikasema, Ee Bwana, Mungu mkuu, mwenye kutisha, ashikaye maagano na rehema kwao wampendao, na kuzishika amri zake; 
5 tumefanya dhambi, tumefanya ukaidi, tumetenda maovu, tumeasi, naam, hata kwa kuyaacha maagizo yako na hukumu zako; 
6 wala hatukuwasikiliza watumishi wako, manabii, ambao kwa jina lako walisema na wafalme wetu, na wakuu wetu, na baba zetu, na watu wote wa nchi. 
7 Ee Bwana, haki ina wewe, lakini kwetu sisi kuna haya ya uso, kama hivi leo; kwa watu wa Yuda, na kwa wenyeji wa Yerusalemu, na kwa Israeli wote, walio karibu na hao walio mbali, katika nchi zote ulikowafukuza, kwa sababu ya makosa yao waliyokukosa. 
8 Ee Bwana, kwetu sisi kuna haya ya uso, kwa wafalme wetu, na wakuu wetu, na baba zetu, kwa sababu tumekutenda dhambi. 
9 Rehema na msamaha ni kwa Bwana Mungu wetu, ingawa tumemwasi; 

Wiki hii na wiki iliyopita tumejifunza kuhusu maombi. Maombi ni muhimu sana katika maisha ya Mkristo. Katika Biblia tunasoma maelezo mengi kuhusu maombi. Pia kuna mifano ya maombi ya watu mbalimbali. Hapo juu ni mfano wa maombi ya Danieli. Tunaweza kujifunza mambo mengi kuhusu Maombi kupitia maombi ya Danieli.

Danieli alimsifu Mungu na alitubu dhambi za Waisraeli. Sisi tunapaswa kuanza sala zetu na toba na kumsifu Mungu kabla kuomba kwa mahitaji wetu.