Date: 
10-10-2018
Reading: 
Acts 3:1-10 (Matendo 3:1-10)

WEDNESDAY 10TH OCTOBER 2018 MORNING                            

Acts 3:1-10 New International Version (NIV)

Peter Heals a Lame Beggar

1 One day Peter and John were going up to the temple at the time of prayer—at three in the afternoon. Now a man who was lame from birth was being carried to the temple gate called Beautiful, where he was put every day to beg from those going into the temple courts. When he saw Peter and John about to enter, he asked them for money. Peter looked straight at him, as did John. Then Peter said, “Look at us!” So the man gave them his attention, expecting to get something from them.

Then Peter said, “Silver or gold I do not have, but what I do have I give you. In the name of Jesus Christ of Nazareth, walk.” Taking him by the right hand, he helped him up, and instantly the man’s feet and ankles became strong. He jumped to his feet and began to walk. Then he went with them into the temple courts, walking and jumping, and praising God. When all the people saw him walking and praising God, 10 they recognized him as the same man who used to sit begging at the temple gate called Beautiful, and they were filled with wonder and amazement at what had happened to him.

 

We have read about a miracle of healing performed by the Apostle Peter. He did not do this by his own power but in the  name of Jesus Christ. It is the type of miracle which Jesus performed many times when He was on earth. Peter had faith that Jesus would heal the man. The man also had faith to believe what Peter said and to stand up and then begin walking and jumping. He was full of joy and he praised God for his healing.

Thank and praise God for all the good things which He is doing in your life even if they are not so dramatic as this miracle.

JUMATANO TAREHE 10 OKTOBA 2018 ASUBUHI                      

MATENDO 3:1-10

1 Basi Petro na Yohana walikuwa wakikwea pamoja kwenda hekaluni, saa ya kusali, saa tisa. 
Na mtu mmoja aliyekuwa kiwete toka tumboni mwa mamaye alichukuliwa na watu, ambaye walimweka kila siku katika mlango wa hekalu uitwao Mzuri, ili aombe sadaka kwa watu waingiao ndani ya hekalu. 
Mtu huyu akiwaona Petro na Yohana wakiingia hekaluni aliomba apewe sadaka. 
Na Petro, akimkazia macho, pamoja na Yohana, akasema, Tutazame sisi. 
Akawaangalia, akitaraji kupata kitu kwao. 
Lakini Petro akasema, Mimi sina fedha, wala dhahabu, lakini nilicho nacho ndicho nikupacho. Kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, simama uende. 
Akamshika mkono wa kuume, akamwinua, mara nyayo zake na vifundo vya miguu yake vikatiwa nguvu. 
Akaondoka upesi akasimama, akaanza kwenda; akaingia ndani ya hekalu pamoja nao, akienda, akiruka-ruka, na kumsifu Mungu. 
Watu wote wakamwona akienda, akimsifu Mungu. 
10 Wakamtambua, ya kuwa yeye ndiye aliyekuwa akiketi na kuomba sadaka penye mlango Mzuri wa hekalu; wakajaa ushangao wakastaajabia mambo yale yaliyompata. 

Hapo juu tunasoma muujiza wa uponyaji ambao Mtume Petro aliwezeshwa kutenda. Petro hakuponya kiwete kwa nguvu zake mwenyewe, bali alikiri alimponya kwa nguvu ya jina la Yesu Kristo. Petro alikuwa na imani kwamba Yesu atamwezesha kuponya mgonjwa. Na mgonjwa aliamini pia. Alikuwa na ujasiri kusimama na tena kutembea na kurukaruka. Aliamini kwamba alipona kabisa. Pia alikuwa na furaha sana na alimsifu Mungu.

Mshukuru Mungu kwa mambo yote mema amekutendea hata kama siyo muujiza kama hili.