Date: 
23-01-2018
Reading: 
2 Corinthians 3:4-11 (2 Wakorintho 3:4-11)

TUESDAY 23RD JANUARY  2018 MORNING                   

2 Corinthians 3:4-11  New international Version (NIV)

Such confidence we have through Christ before God. Not that we are competent in ourselves to claim anything for ourselves, but our competence comes from God. He has made us competent as ministers of a new covenant—not of the letter but of the Spirit; for the letter kills, but the Spirit gives life.

The Greater Glory of the New Covenant

Now if the ministry that brought death, which was engraved in letters on stone, came with glory, so that the Israelites could not look steadily at the face of Moses because of its glory, transitory though it was, will not the ministry of the Spirit be even more glorious? If the ministry that brought condemnation was glorious, how much more glorious is the ministry that brings righteousness! 10 For what was glorious has no glory now in comparison with the surpassing glory. 11 And if what was transitory came with glory, how much greater is the glory of that which lasts!

The New covenant in Jesus Christ is truly glorious.  We thank God that Jesus Christ Himself came to earth to save us from our sins.

We have been saved by faith in Jesus Christ and given the gift of the Holy Spirit to live within us and to guide and sanctify us.  Praise the Lord.

JUMANNE TAREHE 23 JANUARI 2018                            

2 WAKORINTHO 3:4-11

Na tumaini hilo tunalo mbele za Mungu kwa njia ya Kristo. 
Si kwamba twatosha sisi wenyewe kufikiri neno lo lote kwamba ni letu wenyewe, bali utoshelevu wetu watoka kwa Mungu. 
Naye ndiye aliyetutosheleza kuwa wahudumu wa agano jipya; si wa andiko, bali wa roho; kwa maana andiko huua, bali roho huhuisha. 
Basi, ikiwa huduma ya mauti, iliyoandikwa na kuchorwa katika mawe, ilikuja katika utukufu, hata Waisraeli hawakuweza kuukazia macho uso wa Musa, kwa sababu ya utukufu wa uso wake; nao ni utukufu uliokuwa ukibatilika;
je! Huduma ya roho haitazidi kuwa katika utukufu? 
Kwa maana ikiwa huduma ya adhabu ina utukufu, siuze huduma ya haki ina utukufu unaozidi. 
10 Maana hata ile iliyotukuzwa haikuwa na utukufu hivi, kwa sababu ya utukufu uzidio sana. 
11 Kwa maana, ikiwa ile inayobatilika ilikuwa na utukufu, zaidi sana ile ikaayo ina utukufu. 

Agano jipya kweli ni tukufu. Ni ya neema sana Mungu mwenyewe Yesu Kristo aje duniani kutuokoa. Yesu Kristo aliacha utukufu wa mbinguni na kuvaa ubinadmu na alitufia msalabani. Ni kwa neema sana tumeokolewa. Pia tulipewa zawadi ya Roho Mtakatifu kuishi ndani yetu na kutuongoza na kututakasa. Tumsifu Mungu.